Romans 16

Salamu Kwa Watu Binafsi

1 aNapenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea. 2 bNaomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.

3 cWasalimuni Prisila
Prisila kwa Kiyunani ni Priska, hivyo tafsiri nyingine zimemuita Priska.
na Akila, watumishi wenzangu katika Al-Masihi Isa.
4Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu; wala si mimi tu ninayewashukuru bali pia makanisa yote ya watu wa Mataifa.

5 eLisalimuni pia kanisa linalokutana nyumbani mwao.
Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Al-Masihi huko Asia.
6Msalimuni Maria, aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu.
7 fWasalimuni Androniko na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, nao walikuwa katika Al-Masihi kabla yangu.
8Msalimuni Ampliato, yeye nimpendaye katika Bwana.
9 gMsalimuni Urbano, mtendakazi mwenzetu katika Al-Masihi, pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi.

10 hMsalimuni Apele aliyejaribiwa na akaithibitisha imani yake katika Al-Masihi.
Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Aristobulo.

11 iMsalimuni ndugu yangu Herodioni.
Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Narkisi walio katika Bwana.

12 Wasalimuni Trifaina na Trifosa, wale wanawake wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana.
Msalimuni rafiki yangu mpendwa Persisi, mwanamke mwingine aliyefanya kazi kwa bidii katika Bwana.
13 jMsalimuni Rufo, mteule katika Bwana, pamoja na mama yake, ambaye amekuwa mama kwangu pia.
14Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao.
15 kWasalimuni Filologo, Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watakatifu wote walio pamoja nao.

16 lSalimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu.
Makanisa yote ya Al-Masihi yanawasalimu.

Maelekezo Ya Mwisho

17 mNdugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza. 18 nKwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Al-Masihi, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga. 19 oKila mtu amesikia juu ya utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu.

20 pMungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi.

Neema ya Bwana wetu Isa iwe nanyi. Amen.

21 qTimotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu.

22Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana.

23 rGayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu.

Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu.

[
24 sNeema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi iwe pamoja nanyi nyote. Amen.]

Maneno Ya Mwisho Ya Kumsifu Mungu

25 tSasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Isa Al-Masihi, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. 26 uLakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii 27 vMungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Isa Al-Masihi utukufu ni wake milele na milele! Amen.
Copyright information for SwhKC